57. JINSI YA KUZUIA NYWELE KUKATIKA OVYO


Nywele kukatika imekua ni kero kwa watu wengi sana; hasa kwa wanaojali muonekano wa nywele. Nywele zote hukatika (nywele asilia-Natural hair, na nywele zenye dawa-relaxed hair) lakini kiwango ca kukatika hutofautiana kulingana na vitu mbalimbali. Leo tutaangalia sababu za nywele kukatika na njia mojawapo (home made remedy) ambayo mtu yeyote anaweza kutumia na kuzuia nywele kukatika. Angalia mfano wa nywele ambazo hazikatiki zinavovutia.

SABABU ZA NYWELE KUKATIKA
-Matunzo duni
Hii ni pamoja na kukaa na nywele chafu, zenye vumbi au mba na kutozisafisha mara kwa mara.
-Kutumia chanuo au kitana chenye ncha kali
-Matumizi ya drier au moto mara kwa mara kukausha nywele zako.
-Stress/ Msongo wa mawazo
-Mabadiliko ya hormones hasa kwa wanawake waliojifungua, wanaonyonyesha, wanaotumia vidonge vya uzazi mpango na wale wenye umri mkubwa (waliofikia menopause stage).
-Ukosefu wa protein ya kutosha (kwenye mlo pamoja na kwenye steamings).
-Ujauzito ambao hupelekea mtu kuwa na stress ambapo wengi baada ya kujifungua tatzo huwa linaisha.
-Anaemia

SULUHISHO LA MATATIZO HAYO
-Muone daktari kwa matatizo ya stress (kisaikolojia)
-Tumia shampoo yenye virutubisho vya asili, isiyo na viambata sumu kama vile paraben, chumvi na sulphates.
-Hakikisha unapata mlo kamili (Chakula chenye virutubisho vyote ambavyo huchangia katika ukuaji wa nywele).
-Kunywa maji mengi na pata muda wa kutosha kupumzika.

NJIA MOJAWAPO UNAYOWEZA KUTUMIA KUPUNGUZA TATZO HILO
Hii inatumika kwa nywele za asili tu (ambazo hazina dawa).
MAHITAJI
🧚🏻‍♂️Tangawizi vipande 3
🧚🏻‍♂️Mafuta vijiko viwili
🧚🏻‍♂️Maji robo lita

JINSI YA KUTUMIA
-Chukua tangawizi isage ilainike vizuri
-Weka maji robo lita pamoja na mafuta ,hakikisha tangawizi iliyosagwa imechanganyika vizuri na maji yako .
-Chuja vizuri ,kisha paka kichwani hakikisha unapaka hadi kwenye ngozi ya kichwa..
-Vaa kofia ya plastic kwa saa 1 au zaidi
-Osha nywele zako vizuri kwa shampoo
-Tumia mara moja kwa wiki 2 kwa matokeo mazuri zaidi.

NB: Njia hii inazifanya nywele zako ziwe imara, nyeusi na ndefu zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post