59. KUMBUKA: BIDHAA PEKEE HAZIKUZI NYWELE

Kitu ambacho watu wengi wanaotunza nywele wanatakiwa kujua ni bidhaa pekee haziwezi kukuza nywele, hata mtu anunue bidhaa za gharama kiasi gani lakini kama hazitunzi vizuri nywele zake na yeye mwenyewe hajitunzi kiusahihi (kulingana na matakwa ya ukuaji wa nywele) basi itakua ni kazi bure tu. Bidhaa za nywele hazikuzi nywele lakini zinachofanya ni kudumisha nywele zisikatike, kuzifanya ziwe imara, kusupport, kuzishika nywele vizuri wakati wa kustyle, kuzifanya zing'ae vizuri na kuchanika vizuri nk lakini nywele zinakua kutokea ndani.

Hivyo ili nywele ziweze kukua na kuwa ndefu lazima uzingatie vitu viwili vya muhimu;
1. Nywele zinazoota (New growth) ziwe na afya na kukutana na mazingira mazuri ya kichwa.
2. Kuzuia nywele zilizopo kukatika (Lengh Retention).

MAMBO YA MUHIMU YA KUJIFUNZA
Nywele zinatoka ndani ya fuvu la kichwa (scalp) hivyo kitu kinachopakwa nje hakiwezi kufanya nywele zikue sana au vizuri. Hivyo nywele zinahitaji chakula kutoka ndani kwa kufanya yafuatayo;
-Kula mlo kamili
-Kuepuka stress/msongo wa mawazo
-Kunywa maji ya kutosha
-Kutumia hair supplements
-Kupata muda wa kutosha kupumzika

-Bidhaa zinazopakwa nje zinasaidia tu kusupport nywele ziendelee vizuri lakini kinachofanya nywele zikue vizuri ni mwenendo wa maisha ya kila siku. Kitu cha muhimu zaidi ni kutunza ngozi ya kichwa maana ndio inayopokea nywele fresh kutoka ndani.

-Bila kusahau nywele inakua kwa 0.5-1.5inch kwa mwezi inategemea na genes za mtu (biologically), hiyo ndio iko hivo huwezi kufanya zikue haraka zaidi ila kinachotakiwa ni kuzitunza zile zilizopo ili zisikatike

NYWELE NZURI NI MATUNZO.




Post a Comment

Previous Post Next Post