Picha hii inaonesha tofauti kati ya nywele iliyoharibika (Damaged hair) na nywele nzuri zenye afya (Healthy hair)
Katika utunzaji wa nywele asili, adui mmojawapo anaeweza kuziharibu nywele zako na kufanya usipate matokeo mazuri na kufanya nywele za zisipemdeze ni matumizi ya moto; iwe katika kukausha, kunyoosha au kuset. Kama unataka nywele ndefu za asili, inabidi uanze kujifunza jinsi ya kurefusha nywele zako na kutunza nywele zako. Leo nakupa siri kadhaa za kuzingatia ili kukuza nywele zako kiusahihi zaidi na kupata matokeo unayoyapenda.
– Nywele sio asili ya mtu: Sio lazima uwe ‘point 5’ au mtu mweusi wa Marekani kuwa na nywele ndefu. Watanzania wengi wana nywele ndefu, sema wanajua jinsi ya KUTUNZA NYWELE BILA KUZIHARIBU.
– Usitumie moto kali: Kama unapenda kunyosha nywele zako, usitumie dryer sana kwasababu nywele zako zitakatika. Kama ni lazima utumie blow dryer, tumia setting ya baridi ili nywele zako zinyoke.
– Tumia mafuta mazuri: Tumia mafuta mazuri ya kukuza nywele zako pamoja na routine nzuri ya kuzitunza nywele zako. Kama unataka nywele ziwe ndefu, paka mafuta kwanza kwemye ngozi ya kichwa, suka mabutu kabla kulala, na uzipe nywele unyevu mara kwa mara.
-Usiache nywele muda mrefu bila kusuka hii ni kuzuia nywele zisipigwe na upepo sana hivyo kuzuia kujifunga na kukatika pia
– Tumia shampoo nzuri isiyo na viambata sumu kama salts, paraben na sulphates. Shampoo inasaidia kusafisha ngozi ya nywele ili nywele zako zikue haraka.
KUZA NYWELE ZAKO KIASILI, KIUSAHIHI NA SALAMA ZAIDI
Tags:
Hair and Styles