🍀Utaratibu wa kuosha nywele unaweza kuchangia nywele kukatika au kuto kukua vizuri hivo kabla sijaanza kufundisha steaming ni nini au protein ni nini basi tujifunze kuosha nywele zetu kwanza.
HATUA
🍫Step 1: Kama umesuka nywele fumua kisha detangle(kuachanisha vizuri kwa vidole ama chanuo pana)baada ya kuachanisha vizuri unaweza ku tumia detangle cream, spray au leave in conditioner( sio muhimu sana) kisha suka mabutu makubwa ama twist kama una nywele ndefu Kama una nywele fupi acha.
🍫Step 2: apply mafuta ya kukuza nywele(growth oil) kama coconut oil, shime oil, , jojoba oil, castor oil, black seed oil, avocado oil au essential oil make sure ni kimiminika step hii inasaidia ngozi isikaukiwe na mafuta na ina act kama pree_poo(pree_shampooing) na unapaka zikiwa hivo zimesukwa.
🍫Step 3: osha kwa free sulphate shampoo hapa ziko nyingi inategemeana na brand gani utanunua osha vizuri ukiwa umezisuka kisha kausha kwa khanga au shati na kama utatumia taulo basi usisugue kalisha tu kichwani, pia kwenye kuosha waeza oshea maji ya vugu vugu kulingana na hair porosity yako.
🍫Step 4: weka steaming yako au protein treatment kulingana na ratiba yako vaa mfuko wa plastic kisha funga kiremba juu upate joto vizuri kama steaming yako ni ya saa moja,nusu saa au dakika 45 kaa mda huo kisha toa, osha kwa maji ya baridi kisha kausha.
🍫Step 5: paka mafuta yako kisha paka leave in conditioner au paka leave in cinditioner( kama bamia, alovera, flaxseed au za dukani nitakuja kufundisha) kisha mafuta.
🍫Step 6: suka nywele yoyote kama ya uzi au ya mkono, pia pendelea kulala na kitu kichwani hususani iwe na material ya satini.
Tags:
Hair and Styles