Katika kushauriwa ukuzaji wa nywele nzuri na zenye afya mara nyingi tunakuta tunaambiwa tukate ncha za nywele, lakini kukata ncha hizi za nywele kunasaidia vipi kukuza nywele? na je ni mara ngapi unatakiwa kukata hizi ncha?
TUJIFUNZE KIDOGO.....
Ncha za nywele ni zile nywele zilizopo mwishoni kabisa hizi huwa nyepesi kuliko nywele zote ni kama zimesha kufa, wengi hujiuliza kwanini nywele hizi ni nyepesi?
👉🏻 Ni kutokana na matumizi ya moto na kuchana nywele vibaya, hivyo ili kukuza nywele zako kuwa ndefu na zenye afya ni vyema ukakata ncha. Ni kama katika kukata miti au michongoma ile ya juu hukua nakuwa mibaya wakati huku chini inashamiri kwa kupata matunzo mazuri lakini kama utaiacha ile ya juu basi itaharibu show nzima ya hii ya chini.
👉🏻Ncha za nywele mara nyingi huwa zimechoka na hata rangi yake kubadilika, mara nyingi ncha huwa lighter kuliko nywele za chini, zina haribu muonekano mzuri wa nywele
👉🏻 Hata ukitumia pesa kiasi gani katika salon kama ncha za nywele zako hujakata zitaonekana lifeless hazitopendeza hata kidogo lakini pia husababisha ukatikaji wa nywele.
👉🏻Pia huwezi kutibu Ncha kwa kufanya hair treatments, unachotakiwa kufanya ni kuzikata tu, utapoteza muda na fedha zako bure, split ends hazina tiba
JINSI YA KUEPUKA NCHA ZA NYWELE AU NYWELE KIUJUMLA
👉🏻Kata ncha
👉🏻Paka mafuta nywele zako kabla ya kuziosha
👉🏻Chana nywele zako taratibu
👉🏻Tumia chanuo lenye meno makubwa kuchana nywele
👉🏻Punguza matumizi ya moto katika nywele
👉🏻Kula chakula bora na kunywa maji ya kutosha
Tags:
Hair and Styles