UMUHIMU WA LEAVE IN CONDITIONER KWENYE NYWELE ZA ASILI

Leave in conditioner ni moja kati ya bidhaa za nywele ambazo zimekua hazipewi kipaumbele sana na watunzaji wa nywele natural.


🌿Leo napenda kuongelea kuhusu leave in conditioner. 

-Je ni kwanini nywele yako inahitaji leave in conditioner?

- Wengi tumeshindwa kutunza nywele zetu kwa sababu tunaacha kutumia leave in conditioner kwenye nywele zetu.


Vitu vya muhimu kuzingatia siku ambayo unaosha nywele zako.


🍒Kufanya prepoo

🍒Kuosha nywele

🍒Kufanya steaming

🍒Kuosha vizuri kwa kutumia sabuni(shampoo)

🍒Unapaka leave in conditioner yako(bamia au aloe vera)

🍒Kupaka mafuta(growth oil)

🍒Kupaka sealant (Castor Oil au shea butter)

🍒Kusuka style unayoipenda


Sasa shida inakuja pale tunapoenda saloon. -Wengi wetu tukishakuoshwa nywele zetu kinachofuata tunakupakwa (pink lotion) au mafuta ya mgando(blue magic, avocado, sulpher na mengine mengi) na baada ya hapo kifuatacho browdryer kwakua nywele imeshakakamaa haichaniki sasa inabidi tuu moto uhusike🥵


🍒Sasa tunatakiwa tuelewe kuwa leave in conditioner ni ya muhimu na inafanyika mara tuu baada ya kuosha nywele kwasababu:


🍒Inasaidia kuweka unyevu na kulaianisha nywele.


🍒Inasaidia kwenye kuchambua nywele*


🍒Mwisho wa siku tutaishia tuu kuona nywele zinakakamaa, zinakua ngumu hatuwezi kuzihudumia kumbe tumekosea wenyewe.


🌷ZINGATIA LEAVE-IN CONDITIONER NI MUHIMU SANA KILA UNAPOMALIZA KUOSHA NYWELE USIACHE KUPAKA BAMIA AU ALOE VERA KABLA HAUJAPAKA MAFUTA YAKO NA KUSUKA.


NI MUHIMU SANA🥰🥰

Post a Comment

Previous Post Next Post