Tuangalie kwanza matatizo ambayo ambayo wengi wetu imekuwa changamoto hadi kufikia hatua ya kukata tamaa, kunyoa nywele au kuzichoka.
Vitu ambavyo hufanya nywele kukatika
💚Kuwa na ratiba mbaya katika kuzihudumia nywele zetu,hapa watu wengi tumeshindwa tunawezaje kupanga ratiba ya kutunza nywele, kuanzia kuosha,kuzipa unyevu,bidhaa nzuri za kutumia ambazo hazina kemikali (Bad products lead to damaged hair).
Moto wa drier
Overdose heat inasababisha nywele kukatika hasa kwa wale ambao kila week lazima aende kublowdry nywele,lazima aende kupass nywele zake,..Kuwa na nywele zenye afya kunahitaji kuacha kabis matumizi ya moto,moto hukata nywele,kuzifanya dhaifu na kupelekea kuwa nyepes(Wenye nywele za asili),Hata wenye dawa ukipunguza matumizi ya moto utaipenda na kufurahia nywele zako.
Misuko inayopelekea nywele kukatika,
Wote tunajua kuna misuko sio rafiki kwa nywele zetu,kukazwa au kuvutwa hupelekea nywele kukatika hvyo kuacha kukua kabisa,Epuka mitindo kinga migumu kwa nywele zako
Chakula
Panga ratiba ya vyakula vyako vyenye kurutubisha mwil na nywele zako,kunywa maji angalau glass 8 kwa siku.
Kuzipa nywele unyevu
Hii ni muhimu sana kila mtu lazima aitie akilini,nywele kavu hukatika na nywele kavu hutokana na kutokuwa na unyevu,zipe nywele unyevu angalau mara tatu kwa week, seal in moisture (paka vitu ambavyo vitaweza kuweka unyevu ukae muda mrefu kama vile shea butter au Black castor oil) .unaweza tumia njia ya Spray bottle kuweka maji,leave in conditioner,mafuta ya asili au hata maji ya mpera kiasi na ukanyunyizia nywele zako,unaweza tembea nayo hyo chupa maana ni ndogo tu unaweza weka kwenye handbag iwe kama dawa,asubuhi mchana na usiku😀.
ITAENDELEA....
Tags:
Hair and Styles