44. VITU VYA MUHIMU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA, KUSUKA MSUKO KINGA (PROTECTIVE STYLE)

VITU VYA MUHIMU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA, KUSUKA MSUKO KINGA (PROTECTIVE STYLE)
Protective style kwa kiswahili ni Msuko kinga, huu unasukwa ili kuzikinga nywele za asali au za dawa kukatika, kuharibika na hivyo kuzifanya zikue vizuri na zisiwe nausumbufu wowote.

🧚‍♀️Msuko kinga au protective style ni  msuko ambao unaweza kukaa kichwani kwako kuanzia siku tano na kuendelea, mpaka mwezi inatokana na aina ya nywele.

Msuko kinga (Protective style) unaweza kuwa;
🍃 Nywele za rasta (box braids)
🍃Nywele za  mkono (flat twist)
🍃Nywele  za uzi (african threads) nk.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUSUKA
🧚‍♀️Osha nywele zako kwa shampoo;  Unashauriwa utumie sulfate free shampoo.
(Kwa nini utumie  sulfate free shampoo nilifundisha, post zilizopita pitia)
🧚‍♀️Fanya deep conditioner (steaming)
Hii huzuia nywele  kukatika, inakuza nywele na kufanya nywele ziwe na afya; Utakaa na steaming ndani ya nusu saa au dakika 30.
🧚‍♀️Detangle nywele zako ipasavyo
🧚‍♀️Chana  nywele zako kuanzia  juu kushuka chini,wengi tumezoea kuchana kuaanzia chini kupanda juu lakini hii ina madhara mengi kama vile:
-Inasababisha nywele kukatika
-Nywele utaona hazikui
🧚‍♀️Unachana nywele kimafungu kama ni ndefu na nyingi; yaani zilizojaa
🧚‍♀️Hakikisha  unatumia chanuo lenye meno mapana.
🧚‍♀️Moisturize (zipe nywele zako unyevu.
Kwa nini  tunazipa unyevu kwa sababu nywele kavu ni rahisi kukatika,huwa ngumu na kuuma pia.
🧚‍♀️Baada ya hapo suka  msuko wako.

Post a Comment

Previous Post Next Post