4. VITU MUHIMU KATIKA UTUNZAJI WA NYWELE

5. Conditioner (Antie Jackies) na Deep conditioner (Cantu)
Hii ni moja ya product muhimu sana katika kutunza nywele iwe ni za asili au zenye dawa. Kama ambavyo mwili unajitaji chakula cha aina tofauti tofauti vivyo hivyo kwenye nywele pia. Deep conditioner na conditioner  ni chakula cha nywele ambacho kinazifanya nywele ziweze kukua vizuri zikiwa zina afya na nzuri.
Conditioner inaoshwa baada ya muda mfupi sana (chini ya dakika 20) lakini deep conditioner inakaa muda mrefu kwenye nywele, kuanzia dakika 30 na kuendelea. Pia ni vizuri kutumia moisturizer deep conditioner ili unyevu wa nywele usipotee kirahisi.

6. Leave in conditioner
Hizi zipo ambazo ni za kutengeneza mwenyewe nyumbani mfano Rojo ya bamia au aloevera(nitaelekeza jinsi ya kutengeneza huko mbeleni) na za kununua (za kiwandani) mfano Antie Jackie’s na Cantu Leave in conditioner. Hii inatumika baada ya kuosha nywele na kupaka mafuta ili kuzipa nywele unyevu.

7. Butters/Hair cream  (mfano shea butter)
Hizi zinapakwa baada ya kupaka leave in conditioner pamoja na mafuta ya nywele  ili kuseal in moisture (au unyevu) usitoke kirahisi. Hii inafuata mpangilio ufuatao (LOC Method yaani baada ya kuosha nywele unapaka Leave in conditioner (L) halafu Oil (Mafuta ya nywele) mwisho Cream au butter (C).

8. Kitamba cha cotton/microfiber towel
Hiki ni kitambaa maalum kwa ajili ya kukaushia nywele, kinakua na uwezo wa kufyonza maji kirahisi bila kukata au kusumbua nywele. Pia unaweza tumia Tshirt ya cotton (chochote unachoweza afford kirahisi). Usijaribu kutumia taulo la kawaida maana linakata nywele wala usitumie dryer mara kwa mara maana nywele inakua dhaifu na ni rahisi kukatika.

9. Steamer (Deep conditioning cap)

 
Hiki ni  kifaa maalumu kwa ajili ya kuzipa nywele joto wakati wa kufanya deep conditioning au kwa  lugha  iliyozoeleka ni Steaming. Hii ni muhimu kwa sababu steaming yako itaingia kwenye nywele vizuri na kwa haraka zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post