20. JINSI YA KUTUNZA NGOZI YA USO

Uzuri wa ngozi sio rangi tu bali ni muonekano wa ngozi yenyewe kwamba ina afya na mng'ao unaoashiria afya njema.
Leo tushirikishane jinsi ya kufanya facial treatment kwa kutumia vitu vya jikoni, ambayo unaweza fanya mara moja kwa wiki au mara moja ndani ya wiki mbili inategemea na muda wako lakini matokeo mazuri lazima uyapate.
MAHITAJI
✨Kiini  cha yai
✨Machicha ya nazi
✨Tango au limao
JINSI YA KUANDAA
⚡️Safisha uso wako kwa maji safi ya vuguvugu.
⚡️Kama una ngozi kavu au ya kati chukua kipande cha tango kidogo na upake maji yake usoni na kwa wenye ngozi ya mafuta unaweza kutumia kipande cha limao kwa kupaka maji yake.
⚡️Chukua pamba au kitambaa laini na futa maji ya tango au limao usoni taratibu.
⚡️Chukua machicha ya nazi na anza kuusugua uso na shingoni taratibu mpaka uridhike uso wote umepitiwa na machicha yako hasa unapoona unang'aa kwa mafuta kidogo yaliyotoka kwenye nazi.
⚡️Kisha pukuta yale machicha ubaki na uso unaong'aa bila vitu vyeupe yaani machicha.
⚡️Chukua kiini cha yai la kienyeji, au la kisasa lenye kiini cha njano iliyokolea.
NB: Ili kiini kisijichanganye na ute wakati wa kupasua ,ligonge yai upande mmoja sio katikati na limimine kwenye sahani ambayo unaona kiini katikati kisha unakichota na kuweka kando.
⚡️Paka  ule uji mzito wa njano wa kiini uso mzima bila kusahau shingoni na nyuma ya masikio na ngozi ya masikio.
⚡️Baada  ya kupaka kiini cha yai unaweza kuendelea na shughuli zako huku likiendelea kukauka,linapokauka ngozi yako inakuwa kama inajivuta vuta.
⚡️Baada  ya kule kuvuta kuisha inamaanisha yai limekauka kabisa.
⚡️Osha uso wako kwa maji safi na maji yawe ya baridi sasa.
UMUHIMU WA KILA HATUA
Kuosha uso kwa maji ya vuguvugu hufungua matundu ya ngozi.
✨Tango au limao hutumika kama cleanser unapokuja kujifuta taratibu unaondoa uchafu katika ngozi yako.
✨Machicha ya nazi yanatumika kama scrub, yanaondoa seli zilizokufa, kuifanya ngozi kuwa laini na kuipa mngao.
✨Kiini cha yai hapa kinatumika kama maski, matundu ya ngozi yanajifunga vizuri na kinaipa ngozi yako lishe kutokana na vitamins zilizomo kwenye kiini cha yai kama vitamin E.
✨Mwishoni unanawa na maji baridi ili kuruhusu matundu ya ngozi kujifunga na kuifanya ngozi ijiweke sawasawa.
FAIDA ZAKE
Husaidia kutibu na kuikinga ngozi na chunusi
✨Kuipa ngozi mng'ao bila kutumia kemikali za sumu
✨Husaidia kupunguza mikunjo ktk ngozi yako(wrinkles zinapungua)
✨Gharama ndogo kuifanya

Post a Comment

Previous Post Next Post