6. STEAMING/DEEP CONDITIONER/PROTEIN TREATMENT/HAIR MASK

Haya yote ni majina ambayo yanamaanisha kitu kimoja ambacho ni kuzipa nywele zako chakula (kama ilivyo mwili unahitaji chakula cha aina mbalimbali or lets say mlo kamili ili kuwa na afya njema vile vile nywele zinahitaji chakula ili zinawiri na kukua vizuri)

TOFAUTI KATI YA STEAMING YA KAWAIDA NA PROTEIN TREATMENT
🍃Steaming ya kawaida inafanyika kulingana na muda wa mtu inaweza kuwa kila baada ya wiki moja au mbili au kila jmoc inategemea na ratiba ya mtu LAKINI Protein treatment inafanyika kila baada ya mwezi au wiki sita (kama lilivyo jina lake lazima icontain vitu vyenye protein kama vile mayai, mayonisse, parachichi and the like.)

🍃Kwa nn ifanyike kila baada ya mwezi au wiki sita?
Kama tunavojua kila kitu kikipita kiasi kina madhara directly or indirectly, vile vile kweny nywele protein ikizidi nywele zinakua dhaifu au laini mno ambapo zitakatika kirahis mno.

🍃Steaming au protein treatment inawekwa kwenye nywele safi, baada ya kuosha nywele na kuzikausha kidogo ndio unapaka steaming na baada ya nusu saa au lisaa unaosha kwa maji mengi (BILA SHAMPOO) na unapaka leave in conditioner baada ya hapo unapaka mafuta yako ya nywele na mwisho unapaka butter (sealant) ya kushikilia unyevu kweny nywele.

Zipo steamings za aina nyingi sana utakachua unafanya ni kuchagua zile ambazo ni rahisi kwako na vitu vyake ni rahis kupatikana kulingana na sehem ulipo
 MFANO WA STEAMINGS HIZO NI; (ukiona ina yai, mayonisse and sometimes parachichi, hiyo ni protein treatment)
1. Parachichi + ndizi + yai + asali + castor oil
2. Parachichi + Plain yogurt (unflavoured) + asali + limao + castor oil + ute wa bamia
3. Kitunguu swaumu + kitunguu maji + tangawizi + limao + asali + castor oil
4. Maji ya mchele + castor oil + asali
5. Yai + limao/ndimu + castor oil + Vinegar + asali
6. Ndizi + maziwa + asali + castor oil + yai
7. Mtindi + yai + asali + castor oil
8 Mdalasini + castor oil + asali
9. Mchaichai + majani ya mpera + mlonge
10. Maji ya mpera + castor oil + asali
11. Majani ya chai + castor oil/mafuta ya nazi original

Na nyingn nyingi hizi nmeelezea ambazo mtu anaweza tengeneza mwenyewe nyumbani (zipo za kununua kuwa makini na ingredients)

Post a Comment

Previous Post Next Post