29. FAHAMU ZAIDI KUHUSU 4C HAIR TYPE (KIPILIPILI)

Leo tuangalie tabia ya nywele hizo na unachotakiwa kufanya ili kupata matokeo mazuri.
1. Kipilipili
2. Ngumu na nzito
3. Zinajaa sana
4. Zina coils/hair strands zimebanana sana ndio maana nywele zinashikana sana
5. Ina shrink sana (kunywea sana) zaidi ya 70% ya nywele ya kawaida
6. Haina mawimbi hata umwagie maji (labda usuke twists na bantu knots)
7. Ina density kubwa na kujaa sana
8. Ukitaka inyooke na kuwa nzuri suka nywele za uzi au twists mara kwa mara
9.  Hii nywele ni imara sana hivyo inaweza kusukwa au kuwa styled tofauti tofauti na bado ikapendeza bila kukatika
10. Hii ni nywele ambayo inapoteza unyevu kirahs sana hivyo kuipa unyevu inabidi iwe mara kwa mara, pia kuzingatia LOC, LCO methods na variations zake (zitaelezewa kwenye post inatofuata) pamoja na kutumia most of water based products ili kuifanya iwe hydrated most of the times.

NB. Kumbuka mafuta (iwe castor oil, mafuta ya nazi, olive oil n.k) hayawezi kuzipa nywele unyevu na hazina maji pia..sana sana zinaongeza ukavu kwenye nywele.

11. Tumia sana steaming ya bamia, leave in conditioner ya bamia au aloevera products utazipenda nywele zako na zitakua laini.
12. Zingatia sana kudetangle nywele kiusahihi na inaweza chukua muda kuwa straight au kuwa na nafasi kwa sababu zinakua zimejaa.
13. Usitumie moto kabisa iwe kukausha, kunyoosha au kustyle.
14. Panga ratiba ya kutunza nywele zako bila kusahau kuzipa unyevu kila siku
15. Ijue aina ya nywele zako, itunze kwa usahihi na uipende jinsi ilivyo lazima upate matokeo chanya.❤️❤️❤️

Post a Comment

Previous Post Next Post