41. NJIA YA KUKUZA NA KUREFUSHA NYWELE ZAIDI

Najua watu wengi wanapenda kua na nywele nzuri, ndefu na za kuvutia. Waafrika  nywele zetu sio kama za wazungu so zinahitaji matunzo na uangalizi sana ili zirefuke na kuwa nzuri zaidi. Kuna steaming (treatments)  nyingine zinaleta matokeo haraka na nyingine taratibu . Leo tujifunze steaming ya asili yenye matokeo yanayoonekana ya haraka zaidi.

MAHITAJI
🧚‍♀️Ndizi mbivu 1
🧚‍♀️Yai la kienyeji 1
🧚‍♀️Asali(mbichi)-vijiko 5 vya chakula
🧚‍♀️Grand malt-vijiko 10 vya chakula

JINSI YA KUANDAA
🧚‍♀️Safisha ndizi na kumenya vizuri
🧚‍♀️Changanya vitu hivyo vyote kwenye na usage kwenye blender  ili upate uji wake safi.
🧚‍♀️Osha nywele zako kwa shampoo isiyo na viambata sumu
🧚‍♀️Kausha nywele zako kidogo kuondoa maji yanayochuruzika
🧚‍♀️Paka  mchanganyiko huo kichwani
🧚‍♀️ Vaa shower cap nywele iive vizuri.
🧚‍♀️Kaa na shower cap kwa muda wa lisaa limoja.
🧚‍♀️ Osha  nywele zako vizuri kwa kutumia maji tu, bila shampoo
🧚‍♀️Fanya  hivi kila baada ya wiki mbili na baada ya mwezi mmoja utagundua kuwa nyweke zako zimerefuka.

NB: kuna watu watajiuliza yai ni protein iweje unaweka baada ya wiki mbili? Yes ni PROTEIN lakini uwepo wa grand malt (ingredients zake) na asali zinaleta mchanganyiko ambao hata ukitumiwa kila wiki bado hautaleta madhara ya protein nyingi kwenye nywele❤️.

Post a Comment

Previous Post Next Post