Ni kwa muda sasa tumekua tukiongelea njia nzuri na rahisi za kutunza nywele zako za asili, na hakuna nywele ambazo hazina shukurani, labda tu uwe hujatumia bidhaa sahihi kwa aina ya nywele zako.
🍒Katika hali ya kawaida kabisa nywele za kiafrika (Natural hair - 4 type) hukua kwa inch 6 kwa mwaka.
🍒Hivyo unaweza ukajifanyia tathmini kama nywele zako zinakubaliana na hilo au lah. Endapo hazikubaliani na hilo basi kuna sehemu unakosea, inaweza kuwa kwenye;
🌿Products/bidhaa unazotumia
🌿Treatments unazofanya
🌿Kuacha nywele kavu muda mrefu
🌿Nywele kukatika
🌿Magonjwa ya ngozi ya kichwa
🌿Kutumia relaxers kulainisha nywele.
🍒Kwa mantiki hiyo tunategemea kunanzia January hadi June nywele yako ilikua 3 inch na miezi 6 iliyobaki itakua kwa inch 3 vile vile.
🌷Kama hupati matokeo hayo jitathmini unakosea wapi na kuanza kuacha mambo yanayokuchelewesha kukuza na kustawisha nywele zako.
🍒But so far hii ndio njia rahis ya kuelezea ukuaji wa nywele na wengine bado hawajaelewa hapa wanachanganyikiwa kutaka mafuta ya kukuza nywele haraka kila mara na wanasahau msingi wa kukuza nywele ni matunzo yaliyo sahihi.
🍒Ukielewa hii concept vizuri hutaruhusu nywele yako ikatike au kufanya vile vitu vinavyoweza sababisha nywele yako kukatika.
🍒Wengne nywele inakua chini na kukatika juu kwa uwiano sawa kutokana na kutoitunza nywele vizur lakin siku zote anatafuta mafuta ya kukuza nywele ikuwe haraka, hapo unakosea sana maana nywele zako zinakua sawa na zinazokatika hivyo huwezi kuona mabadiliko.
🍒Badili muenendo wako wa kutunza nywele na uanze muenendo wa kutunza nywele ili ziwe na afya hii itakusaidia kila kitu kuhusu namna ya utunzaji wa nywele.
🍒Hivyo usilalamike hili suala tena😂
-Mbona nywele yangu haikui? Kwa sababu nywele zako zinakua lakini zinakatika hivyo huwezi kuona kama zinakua.