🍒Nywele kuwa nyepesi na kukatika ni tatizo sugu kwa baadhi ya watu haswa kwa wanawake.
🍒 Watu wengi wanapoteza pesa nyingi wakihangaika huku na kule kutafuta suluhisho juu ya tatizo hili.
🍒Leo nataka nikujuze namna ya kupambana na tatito hili kwa kutumia tangawizi na kitunguu maji tuu.
🌿Tangawizi na kitunguu maji ni viungo tunavyovitumia jikoni kila siku katika upishi lakini viungo hivi tunaweza kuvitumia pia kwenye nywele kukabiliana na tatizo la nywele kuwa nyepesi na kukatika.
Tangawizi imesheheni madini ya;
🌺Magnesium
🌺Potasium
🌺Phospate pamoja na vitamins ambavyo vinasaidia nywele kuwa zenye afya na hivyo kuzuia kukatika kwa nywele.
🌷Kwa upande wa kitunguu maji kinasaidia kupambana na bacteria wanaoweza kusababisha magonywa ya ngozi ya kichwa kama mba ambayo huchangia kukatika kwa nywele.
🍒Ili kutumia viungo hivi kama tiba kwa nywele zako unatakiwa kusaga tangawizi pamoja na kitunguu maji chako kisha kuvichuja na kupaka mchanganyiko huu kwenye ngozi ya kichwa chako, tumia kofia ya plastiki kufunika nywele zako kwa dakika 15 na baada ya hapo osha nywele zako kwa maji baridi na shampoo kidogo.
Kuna msemo unaosema “Ukitaka kupata mazao mazuri basi andaa ardhi yako vizuri”, vivyo hivyo kwenye nywele ukitaka kuwa na nywele nzuri zenye afya una budi kuandaa ngozi yako ya kichwa vizuri.
❤️❤️