23. HATUA ZA KUFUATA KUANZIA PREPOO HADI KUSUKA AU KUBANA STYLE

HATUA ZA KUFUATA KUANZIA PREPOO HADI KUSUKA AU KUBANA STYLE

1.PREPOO (PRE-SHAMPOO)
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo inafanyika siku moja kabla ya kuosha nywele; Mfano unachagua siku maalumu ya kuosha nywel  nywele zako ambayo ni  Jumamosi,  basi siku ya Ijumaa unafanya PREPOO ikiwa na maana ya napaka mafuta katika ngozi ya kichwa halafu una massage vizuri, na kama hujasuka  unafunga mabutu au kusuka twists kisha unavaa kofia ya satini unalala. Kesho yake (siku  ya pili ambapo kwa case hii ni Jumamosi) unafanya  matayarsho ya HAIR TREAMENT (Hapa itaelezewa Hair treatment ambayo ni PROTEIN TREATMENT).

Mahitaji
🌿Parachichi (avocado) nusu (1/2)
🌿Asali kijiko kimoja
🌿Yai moja
🌿Mafuta kijiko kimoja( Black Castor Oil(Mafuta ya mnyonyo)/Olive oil(Mafuta ya mzeituni/Coconut oil(Mafuta ya nazi)
🌿Mayonisse kijiko kimoja

Jinsi ya kuandaa na kuchanganya
🧚‍♀️Changanya vitu hivyo vyote halafu unasaga  kwa blender
🧚‍♀️Baada ya kupata mchanganyiko mzuri unaviacha pembeni
🧚‍♀️Unaandaa nywele zako kwa ajili ya kuosha
🧚‍♀️Kama ulikua hujafumua  nywele zako unafumua na kufanya  detangling vizuri
🧚‍♀️ Unachukua shampoo (sulfate, paraben and salt free) unapaka katika ngoz na kujimwagia  maji kdogo kichwani
🧚‍♀️Baada ya hapo unaanza kusugua sugua vzuri hadi ukiridhika unasuuza vizuri
🧚‍♀️Kama nywele  zimekatika basi unaxisuuza vzur, halaf unachukua  CONDITIONER halafu napaka katika nywele zote sugua sugua kichwa kizima.
🧚‍♀️Unaacha kama dk 5 ivi halafu unaosha na maji safi tuu
🧚‍♀️ Sasa unachukua HAIR TREATMENT yako unapaka ,halafu navaa shower cap au deep conditioner cap.
🧚‍♀️ Kaa nayo kwa  dk 35 huku unaendelea  na kazi nyingine while  nywele znaiva😊
🧚‍♀️Muda ukifika osha sasa na maji baridi or vuguvugu lakini  usijmwagie maji moto sio mazuri kwa nywele.
🧚‍♀️Baada ya kusuuza unachukua  tshirt  au microfiber towel na kuanza   kukausha

NB: Usitumie TAULO kukaushia nywele  linakata nywele mno.

LOC Method
LOC  method means Leave in conditioner, Oils na Cream
 Jinsi ya kufanya
🌿Baada ya kufuta nywele unachukua leave in conditioner na kupaka nywele zote.
🌿Ukimaliza hapo unapaka mafuta ya maji (ya kimiminika)
🌿Baada ya hapo unapaka  Cream ya Shea Butter unakua umemaliza

🍀Unaweza kwenda kusuka au kustyle nywele unavopenda wewe
☘️Unashauriwa  usisuke nywele zkiwa kavu na wala usichane nywele kavu maana unazikosesha nywele  uhai na zitakatika..

Post a Comment

Previous Post Next Post