26. JINSI YA KUTOA MADOA MADOA YALIYOSABABISHWA NA CHUNUSI

Asilimia kubwa ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na chunusi kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi,  na hii husababishwa  sana na mabadiliko ya miili kipindi cha ujana , au kwa watu wenye nyuso zenye mafuta na baadhi ya watu wamepata matatizo haya  baada ya kutumia baadhi ya vipodozi visivyoendana na ngozi zao.. Leo  tutaenda kuangalia  moja ya tiba ya kuondoa madoa madoa ya chunusi inayoweza kutengenezwa na mtu yoyote nyumbani bila kutumia gharama kubwa.

Mahitaji
⚡Unga wa Riwa
⚡Maji ya Rose (Rose water)
⚡Maji  safi ya kawaida
⚡Limao
⚡Mafuta ya mzeituni (Olive oil)

JINSI YA KUTUMIA
⚡Changanya unga wa riwa na rose water, koroga mchanganyiko huo hadi uwe mzito.
⚡Upake mchanganyiko huo katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke.

NB: Unaweza kukaa na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu  ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya mafuta na kuacha ngozi kavu.

⚡ Nawa  vizuri na maji ya uvuguvugu.
⚡Paka juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu.  Juice  ya limao inatumika kama breach  ya asili ambayo husaidia kufifisha madoadoa  na kuondoa makovu kwenye ngozi .
⚡Paka mafuta ya Olive  kwenye makovu, hii husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.

MAMBO YA KUZINGATIA
💦Wakati unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali
💦. Jaribu kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki  ndani ya mwezi mmoja utaona matokeo yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post