27. LOC METHOD

Leo tujifunze au  tujikumbushie njia mojawapo ya  kutunza au kuhifadhi unyevu kwenye nywele ijulikanayo kama LOC Method - L= Liquid/Leave in conditioner, O = Oil na C=Cream kama picha inavoonesha.

🧚‍♀️LIQUID  mara nyingi inakua ni maji au water based leave in conditioner ambayo ndio unaanza kupaka kwenye nywele zako ili kufungua pores. Pendelea kutumia spray bottle kwan inafanya maji yapenetrate vizuri kuanzia kwenye ncha za nywele mpaka kwenye ngozi. Nywele kikawaida inahitaji moisture au unyevunyevu ili isikatike na unyevu huo hupelekea kuwepo kwa blood circulation sehemu hisia ili nywele ziweze kuota vizuri

🧚‍♀️Baada ya kuspray nywele zako unakuja kwenye step ya pili ambayo ni OIL, hapa unataka mafuta ya maji kama coconut oil, olive oil, jojoba oil, castor oil au hair serum yoyote unampenda kutumia ila iwe katika hali ya kimiminika au liquid form. Oil inasaidia kulock in moisture baada ya kuzispray nywele  zako maji au leave in conditioner au mixer ya hivyo viwili.

⚡️✨Kuna watu wanakimbilia step ya pili ya kupaka mafuta na kuacha step ya kwanza kuspray nywele maji na hapa ndipo watu wengi hukosea na ndio maana ukavu wa nywele zao hauishi,  mtu anaexperience nywele kuwa kavu kila siku pamoja na kuwa anapaka mafuta kila siku na ya kila aina ila nywele bado kavu. Hiyo ni kwa sababu ya kuruka step ya kwanza ambayo hutoa nywele katika hali ya ukavu na kukimbilia step ya kupaka mafuta. Mafuta pekee hawawezi kufanya nywele zako kutokuwa kavu. (Take note kwenye hizo step mbili ni muhimu sana na zifanywe kwa kufuatana).

🔥Na step ya mwisho ni CREAM. Baada ya kuspray nywele zako, ukapaka mafuta ya kimiminika tena hakikisha unapaka kwenye ngozi vizuri mpaka nywele juu kabisa kwenye ncha ndio unakuja kwenye step ya tatu na ya mwishop ya kupaka hair cream. Hair cream inasaidia kuseal in moisture yaan kuhifadhi nywele iwe katika hali ya unyevu unyevu  cream ina boost hair growth na pia insect kama hair protection dhidi ya jua, mvua, tupelo na kitu chochote ambacho kinaweza kuaffect nywele zako. Na cream nzuri hapa kwa nywele zako ni Shea butter au Heavy Jamaican Black castor oil (Castor oil nzito) ila ni vizuri kutumia shea butter coz ni nzito zaidi na ina vitamins nyingi sana za kupost hair growth na kulinda nywele na pia kufanya nywele zako zisiwe kavu kirahisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post