52. AINA ZA LEAVE IN CONDITIONERS

52. AINA ZA LEAVE IN CONDITIONERS
(Za kutengeneza nyumbani/Homemade/DIY)


1.COCONUT MILK LEAVE IN CONDITIONER
🧚🏻‍♂️Nazi ina proteins na Vitaminis inaongeza  uimara na kuchambuka vizuri kwa nywele ambazo zimeharibika kwa njia yoyote ile.

MAHITAJI
🧚🏻‍♂️TUI ZITO LA NAZI
FAIDA YAKE: Sio tu inatibu nywele kavu lakini pia ni kama Deep conditioner/Steaming inayoweka unyevu,kuimarisha nywele zako,inasaidia kulinda na kutibu nywele zinazokatika/kunyonyoka.
🧚🏻‍♂️VITAMIN E OIL
FAIDA YAKE: Husaidia kulainisha nywele,kung'arisha na inafanya kazi kama Preservatives katika mchanganyiko wako huu.
🧚🏻‍♂️LAVENDER ESSENTIAL OIL
Inatumika sana kwenye nywele inasaidia katika ukuaji wa nywele na mambo mengine mengi,hung'arisha nywele na inakupa harufu nzuri.

JINSI YA KUANDAA
🧚🏻‍♂️½ Kikombe cha Tui la Nazi zito (Coconut Milk)
🧚🏻‍♂️1 kikombe Maji (Unaweza Tumia Distilled water,maji maalumu huuzwa kwa kutengenezea vipodozi)
🧚🏻‍♂️1 kijiko cha chai Vitamin E Oil
🧚🏻‍♂️Matone 5 au 10 ya Lavender E.O

Chanya vyote pamoja  na uweke kwenye Pump Bottle tayari kwa Matumizi,

NB: Inaweza Kudumu hata miezi mitatu kama utatumia Distilled water na Ready Made Coconut Milk. Vinginevyo hifadhi katika fridge.

2. BUTTER CREAM LEAVE IN CONDITIONER
 Kuna butter cream tofauti tofauti ambazo zimeshatengenezwa tayari (Ready made)  mfano,Shea Butter,Mango Butter

MAHITAJI
🧚🏻‍♂️ Kikombe kimoja  cha Shea Butter
🧚🏻‍♂️Vijiko vi3 vya chai Mafuta ya Nazi
🧚🏻‍♂️Vijiko vi3 Aloe Vera gel/juice
🧚🏻‍♂️Kijiko ki1 cha Asali/Glycerine 1-2 kijiko cha chai (tsp)

JINSI YA KUANDAA
🧚🏻‍♂️Changanya Pamoja tumia kijiko/mwiko wa mbao,blender au hand mixer ili upate mchanganyiko mzuri (Consistency) na uweke kwenye kopo  lenye mfuniko.
NB: Inadumu muda mrefu tu kwa iyo unaweza tumia hadi mchanganyiko utakapoisha.

3. BAMIA/OKRA LEAVE IN CONDITIONER

MAHITAJI
🧚🏻‍♂️Bamia  changa/teke 3
🧚🏻‍♂️Maji  kikombe kimoja
🧚🏻‍♂️Mafuta yotote (Carrier Oils-mfano Coconut oil, jojoba oil, Castor oil nk) matone 10

JINSI YA KUANDAA.
Kata bamia,weka maji yako chemsha kwa dk 10,halafu  acha ipoe ,chuja upate gel ya bamia ongeza na mafuta matone machache na Utumie.
NB: Shelf Life/ inaweza kukaa hadi wiki 3 ikikaa kwenye fridge. Vinginevyo ni siku moja tu

Post a Comment

Previous Post Next Post